Inawezekana hata wewe unayesoma makala haya unajuta kiasi cha
kulalamikia mwenzako alivyobadilika tabia tofauti na mwanzo ulivyoanza
kupendana naye. Hebu fuatilia dondoo hizi ili ujue namna ya kumtabua
mpenzi anayekufichia makucha, ili usijiingize kwenye uhusiano usiokuwa
sahihi.
MPE UHURU WA KUTOSHA
Watu wengi wanapoanzisha uhusiano huwabana sana wapenzi wao kwa
kuwapekulia simu, kuwachunga watokapo na waingiapo, jambo ambalo
huwafanya wahusika kujilinda sana wakiamini wanafuatiliwa.
Ndugu yangu usimbane mpenzi wako, mwache huru, atembee atakavyo na
awasiliane na amtakaye, wewe kaa nyuma yake ukimchunguza bila mwenyewe
kujua. “Mke/mume wangu hajali mambo haya” Hujali kumbe unamteka mwisho
wa yote utamnasa.
MPE MAJUKUMU
Ukisha mchagua
umpendaye, huwezi kutambua uwezo wake mpaka umpe majukumu ya kufanya.
Kwa mfano mtume akalipie maji, umeme au mwagize asimamie jambo fulani.
Ukishafanya hivyo kaa kando mwangalie, anavyoiba chenji, anavyopunguza
gharama bila kukushirikisha, lakini baadaye muulize, utashangaa
alivyotibua mambo akidhani wewe si mtu wa kujali sana, kumbe ulikuwa
umemtega na hatimaye umemnasa.
MUWEKE KWENYE WAKATI MGUMU
Njia nyingine ya kumnasa anayekufichia makucha ni kumweka katika wakati
mgumu. Wanasema rafiki wa kweli hujulikana kwa dhiki. Tengeneza dhiki
kwa makusudi na kuzitekeleza. Akikuambia naomba unitumie vocha mpenzi au
ninunulie nguo mwambie sina pesa, halafu uone kama atakuwa na kiwango
kile kile cha mapenzi. Wapo wanaume wengine wa pesa na mishahara ya
wapenzi wao, ili kuwabaini ni kuwanyima wakati mwingine.
TUMIA WATU
Katika hali ya kawaida, majirani na marafiki wanawatambua zaidi wapenzi
wetu kuliko jinsi tunavyowatambua sisi. Inawezekana kabisa mpenzi wako
akawa mtakatifu unapokuwepo lakini ukiondoka anajiachia ile mbaya, hivyo
ili kujua tabia zake waulize rafiki na jirani zako watakusaidia
kumtabua mpenzi wako.
ANGALIA ANAVYOWATENDEA WENGINE
Wapenzi wengi wanapokuwa wamepata wapenzi hutazama wanavyotendewa wao na
kudhani inatosha. Mtu muungwana huwatendea wengine mema. “Aa, mama naye
kanichosha kila siku anataka pesa.”
Hebu sikia kauli hii, kama
mtu analalamika kuchoshwa na mama yake itakuwaje kwako? Amka na
kutambua kuwa anakufichia makucha na ipo siku atakubadilikia hata wewe
na kukutesa. Amka usikubali kudanganywa na mpenzi mnafiki.
No comments:
Post a Comment