Friday, November 28, 2014

Kwa wale msiojua nini maana ya ESCROW ACCOUNT fwatilia kwa umakini hii taarifa fupi.

Dar es Salaam. Sakata la tuhuma za wizi wa pesa katika Akaunti ya Escrow ndani ya Benki Kuu (BoT) sasa limehamia mahakamani baada ya Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kumfungulia mashtaka Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi), David Kafulila.


 Kama ilivyotarajiwa na wengi hususani wale wafuatiliaji wa mambo hapa nchini walivyotabili kuwa kafulila hata hafanye nini katika sakata hili la Escrow hataweza kutimiza malengo yake ya kutetea fedha za umma sababu kubwa ikiwa ni moja tu sakata hilo linagusa vigogo wakubwa katika taifa ambao hawako tayari kurudishwa fedha za umma kwa wenyewe,
 Sakata hilo ambalo lililoibuliwa huko bungeni nambunge machachari tokea mkoa wa Kigoma limeshuhudia vigogo wengi wakitoa matamko yao kuhusu sakata hilo wengine wakiita hati za ushahidi zinazotolewa na Kafulila hazina ukweli wowote,kitu ambacho si kweli
 Sakata hilo linalomgusa moja kwa moja mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Mh.EliakimMaswi, linaonekanakuwatete kufuatia hali inavyoendelea kwa sasa kwani sasa sakata hilo limefikishwa mahakamani na kwamba kwa vyovyote vile sasa kafulila atatakiwa kufunga mdomo wake wa kuwaambia wananchi kuhusu kudai fedhazao na hivyo vigogo hao kuendelea kula nchi mpka hapo kesi ya msingi itakapotatuliwa,
wadau wanasema jino moja sababu ikiwa ni kesi yenyewe kugusa maaslahi ya wakubwa ambayo sasa inakuwa vigumu ni nani wa kumfunga paka kengere katika kudai fedha hizo,

Habari kamili ya kupelekwa mahakamani kwa kafulila hii hapa


Kafulila amefunguliwa kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na IPTL kwa kushirikiana na Kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited (mlalamikaji wa pili) na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hizo, Harbinder Sigh Seth (mlalamikaji wa tatu).


Katika kesi hiyo namba 131 ya mwaka 2014, walalamikaji kwa pamoja wanaiomba mahakama imwamuru mbunge huyo awalipe fidia ya jumla ya Sh310 bilioni kwa madai ya kutoa kashfa dhidi yao kwa kuwatuhumu kujipatia pesa kutoka Akaunti ya Escrow, kwa njia zisizo halali.

Kwa nyakati tofauti ndani na nje ya Bunge, Kafulila amekuwa akiituhumu PAP na Seth kuchota Sh200 biloni kutoka akaunti hiyo kupitia IPTL isivyo halali, huku pia akiwataja mawaziri na maofisa wengine wa serikalini kuhusika katika wizi huo.

Maombi ya walalamikaji

Kwa mujibu wa hati ya madai iliyowasilishwa mahakamani hapo, walalamikaji wanaiomba mahakama imwamuru mbunge huyo awalipe Sh210 bilioni kama fidia kutokana na kashfa hizo na hasara ya taswira ya biashara na hadhi yao.

Pia wanaiomba mahakama imwamuru mdaiwa awalipe Sh100 bilioni kama fidia ya madhara ya jumla kutokana na usumbufu walioupata kutokana na taarifa za kashfa zilizotolewa na mdaiwa dhidi yao.

Mbali na malipo hayo ya fidia, pia walalamikaji hao wanaiomba mahakama imwamuru mdaiwa awaombe radhi kutokana na taarifa hizo.

Maombi mengine ni gharama za kesi, riba kwa kiasi cha pesa yote wanayodai kwa kiwango cha asilimia cha mahakama, kutoka tarehe ya hukumu hadi tarehe ya mwisho wa malipo hayo na amri nyingine ambazo mahakama itaona zinafaa.

Inaeleza kuwa kutokana na mgogoro huo, kiasi cha Sh200 bilioni ziliwekwa katika Akaunti ya Escrow iliyofunguliwa BoT, kusubiri kumalizika kwa mgogoro wao huo uliokuwa mahakamani hapo.

Hati hiyo inaendelea kueleza kuwa mgogoro huo ulimalizika na kuhitimishwa kwa mdai wa kwanza (IPTL) kupata amri ya mahakama kumiliki pesa hizo na BoT kutakiwa kuziachia.iv

No comments:

Post a Comment