Wednesday, December 03, 2014

RAIS KIKWETE AMTEUA PRO. ASSAD KUWA CAG MPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba Mosi, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nneasubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.
                             Picha ikimwonyesha Raisi Kikwete katikati na Aliemteuwa kulia kwake.

No comments:

Post a Comment