Friday, November 28, 2014

Kinachoendelea Bungeni Jana

MUHONGO‬ ANASEMA.
DHANA YA MADAI YA BILIONI 321
Madai kwamba IPTL inaidai IPTL 321 Bilioni, bodi ya TANESCO imekana kuyatambua madai haya na vitabu vya TANESCO vinavyokaguliwa na CAG hakionyeshi madai haya.
Madai yaliyowasilishwa na mufilisi, yalitakiwa kuhakikiwa lakini hayakuhakikiwa na hayakuwa na uhalali wowote.
Kamati ya PAC, wamesema yana uhalali japo uhalali wake unategemea maamuzi.
TANESCO kwa kushirikiana na IPTL ilifanya uhakiki ili kujua madai halali ya IPTL kabla ya kufanya malipo. Deni la TANESCO kama capacity charge lilikuwa $370milioni ambazo ni pungufu ya $90 milioni ya madai ya IPTL. Yalifanyika hoteli ya Kunduchi na majina ya waliokuwepo anawataja.
Hizi takwimu zinaonyesha hakuna fedha yetu pale tunayodai bali tunadaiwa na IPTL. Hamna fedha ya umma popote bali tunadaiwa na makampuni ya uzalishaji umeme(anataja makampuni na madeni wanayodai).
Madai yoyote yaliyotokea nje ya nchi laima yasajiliwa nchini, shauri la London haliusiani na fedha za IPTL.
Madai dhidi ya IPTL ikiwemo VAT, serikali ilitaka kinga.
Gharama za mawakili za Mkono adv, hadi hukumu inatoka 2013. TANESCO na serikali zililipa mawakili bilioni 62.9 na bado mawakili hawa wanadai TANESCO $ milioni 4.5 na walipendekeza wapewe kazi nyingine ya kwenda kupinga huku lakini bodi ilikataa kuendelea na hio kazi. Tunajua fika tumepata hasara gani kupitia kampuni ya Mkono.
Kumalizika kwa mgororo na IPTL tumeokoa bilioni 95 za uwakili. TANESCO ilikua na nafasi finyu mno ya kushinda kesi ya London kulingana na ushauri

No comments:

Post a Comment