Monday, December 30, 2013

Wosia wa Jack Cliff kwa Martin Kadinda.


                                           Martin kadinda na Jackie Cliff wakiwa matembezini



                                     Personal Msg kutoka kwa Jackie kwenda kwa Martin Kadinda

 Jackie Cliff na Martin Kadinda ambae ni meneja wa mwigizaji Wema Sepetu ni marafiki wa siku nyingi ambao wamekua wakionekana pamoja kwenye matukio mbalimbali ndani ya  Dar es salaam.
Kutokana na ukaribu wao kama Marafiki pamoja na hili tukio lililomtokea Jackie huko Macao kwa kukamatwa na dawa za kulevya, hii status ya BBM imeonganishwa fasta na kuonekana kama ndio kitu cha mwisho Jackie alichokisema kuhusu maisha yake.
Martin Kadinda amezungumza na kusema ‘hii status kweli ni Jackie aliniandikia lakini sio ya leo, wengi wanadhani ndio kaiandika juzi lakini ukweli ni kwamba aliiandika siku nyingi sana tena hakuwa kwenye matatizo yoyote, kaiandika March 15 2012 ila blogs ndio zimeiunganisha na tukio la juzi’
‘Alisema vitu kadhaa vifanywe akifa na ameguswa na mstari mmoja wa Biblia kwamba ‘inabidi binadamu kukaa tayari wakati wowote maana hatujui siku wala saa’ na kuongeza kuwa kama akizikwa Iringa atapenda azikwe chini ya mti mkubwa wenye kivuli lakini kama atazikwa Dar, msiba uwekwe eneo la ndani lenye AC maana anajua rafiki zake ni watu wenye mashauzi’ – Martin

No comments:

Post a Comment