Friday, December 06, 2013

Haya sasa Bumbuli Kazi kwenu...

 
Wakala wa Taifa wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani Tanga umepitisha maombi ya kupandishwa hadhi barabara zenye urefu wa kilometa 130 zinazounganisha vijiji 9 katika Halmashauri mpya ya Bumbuli. Hii inamaanisha kwamba sasa barabara hizi zitahudumiwa na TANROADS badala ya Halmashauri katika kuziendeleza kwa kiwango bora zaidi.

Barabara hizi zinaunganisha makao makuu ya Bumbuli na halmashauri za wilaya ya Lushoto na Korogwe kupitia kwenye barabara za mkoa za Mombo/Lushoto/Soni/Bumbuli/Dindira na Kwamote pamoja na Mashewa na Bombo Mtoni.

Kupandishwa hadhi kwa barabara hizo kutasaidia usafirishaji wa mazao ya wakulima katika jitahada za kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na hatimaye kuinua maendeleo ya Halmashauri ya Bumbuli kwa ujumla.

Hii ni hatua kubwa na muhimu katika miundombinu kwa Halmashauri yetu mpya ya Bumbuli.

No comments:

Post a Comment