Binti wa miaka 19 ambaye aliacha shule baada ya baba na mama kufa katika
ajali mbaya na ndugu kutompa msaada aliamua kuondoka nyumbani na kwenda
kuishi na kijana mmoja. Miaka 10 sasa amekuwa anakaa na rafiki yake wa
kiume avutaye bangi katika ghetto.
Amekuwa anapewa fedha
kidogo kutoka kwa huyo mpenzi wake ili anunulie chakula na kula na
marafiki wa kaka huyo baada ya kutumika kimapenzi kwa wiki zima huku
akiuza maji ya kunywa.
Baada ya muda akajikuta ni mjamzito na huyo kijana
akamwambia watoe tu mimba hiyo.Akampa fedha kidogo na kumwambia aongeze
nyingine ambazo amekuwa akimpa ili akatoe mimba bila kukumbuka kuwa
fedha hizo zimekuwa zikitumika kwa ajili ya chakula.
Siku ya
pili yake akiwa anatoka chumbani mwao kwenda kutoa mimba, akpita kwenye
korido ambako akakanyanga sakafu ambayo ina maji na kuteleza. yule
kijana akamwona wakati anaangukia tumbo pale sakafuni na akasema, “
amini au usiamini hii ndio njia rahisi niliyoitaka uitumie kutoa mimba
hiyo”
Kijana akamchukua binti wakati huo damu nyingi
zikimtoka na kumwambia aende bafuni akanawe.Lakini kwa nguvu za mwenyezi
Mungu yule dada alipona ingawa mimba ilitoka na akaumwa kwa zaidi ya
wiki bila msaada wowote ule..
Siku moja akiwa anauza maji
akakutana na muuza magazeti na kumpa maji pakiti moja bure na kumwambia,
“leo ni miaka kumi tangu baba na mama yangu wafariki katika ajali
mbaya, hivyo sitajali mchumba wangu atasemaje au kunifanya nini kwa
kutoa maji haya bure, ila mimi nitatoa maji bure kama kumbukumbu ya siku
hii yenye simanzi kwangu”.
Akiwa anataka kuondoka yule muuza
magazeti akamwambia kuwa kuna nafasi ya kazi sehemu na kuwa atamsaidia
kuandika barua ya kuomba. Yule dada ailishukuru na akawa anampigia mara
kwa mara yule muuza magazeti mpaka siku akaitwa kwenda kwenye usaili.
Siku ya usaili akiwa njiani anaelekea huko akakutana na mama mmoja
akiwa na gari aina ya BMW likiwa nimeishiwa mafuta. Yule dada akamuuliza
mama, Je unahitaji msaada gani?
yule mama akamwambia
nimeishiwa mafuta na sijui cha kufanya hapa. Dada akachukua kidumu na
kwenda mbio kumnunulia mafuta yule mama na akarudi na kumpa.
Yule mama alipotaka kumpa hela, dada akakataa akasema nimekuona
nikamkumbuka mama yangu hivyo nimefurahi kukusaidia, kama hutajali
naomba niwahi sehemu.
Kufika kwenye usaili dada akashangaa
kuona kumbe yule mama mwenye BMW ndio boss wa ile kampuni na akafanyiwa
usahili na kuanza kazi na sasa anajimudu kifedha na ana biashara zake.
Na sasa hakai tena na yule kijana mvuta bangi wakati nusu ya utajiri wake anaupeleka kwenye vituo vya kulelea watoto yatima.
Nami leo nakuombea unayeisoma habari hii, Mungu akujalie na
kukufungulia milango ya mafanikio katika kila jaribu unalolipitia na
ukumbuke kuwasaidia wanao hitaji msaada wako.
No comments:
Post a Comment